Imaja centre

Imaja centre

Friday, December 30, 2016

Wanafunzi wote..........IMAJA is wishing you good preparation to embrace new year BUT not forget that on 3thJanuary,2017 we shall resume our study.....ALL THE BEST.

Monday, December 19, 2016

Education gives a way of positive thinking to anyone. Welcome and en light your future at IMAJA

TUNAPOKEA WANAFUNZI SASA

Tumeshaanza kupokea wanafunzi mwaka mpya wa masomo mwaka 2016-2017.
Karibuni sana.

JIENDELEZE KIELIMU

Kama  unahitaji kujiendeleza kielimu kwa kusoma O-level  & Advance(form five&six)karibu sana Imaja Open school kwa elimu bora.
Tunatoa masomo kwa watu wote wanaotaka kujiendeleza/ wanaotaka kurudia mtihani wa QT, kidato cha nne na cha sita. Masomo yote ni kwa mwaka mmoja tu!
Madarasa tulionayo ni kama ifuatavyo:-
  • QT 
  • Form Three & four
  • Form five & Six

Gharama zetu ni nafuu sana. Timiza malengo yako kielimu na Imaja Open School kwa elimu ya uhakika na kiwango bora

Thursday, December 8, 2016

MTAZAMO WA ELIMU.

Leo tutazame katika swala la dhana ya Elimu na maana yake kwa ujumla,je wewe unadhani Elimu ni nini?
Wataalamu na wadau mbalimbali wa Elimu, wametafsiri dhana ya Elimu katika maana tofauti tofauti.kuna waliosema Elimu ni:
*Tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi.
*Ni mchakato mzima unaowezesha kujifunza
*Utajiri wa maarifa anaoupata mtu binafsi baada ya kujifunza mambo fulani,masomo au kupitia michakato ya maisha katika mazingira yake.
Wengine wamedadavua kwa undani zaidi kuwa Elimu ni ukuzaji wa ufahamu wa binadamu (enlightment).Ukuzajiwa ufahamu huu ambao unapaswa kumpelekea binadamu na kumfanya binadamu kutenda katika usahihi , ili kumfanya binadamu awe binadamu bora zaidi na mwenye kuzalisha na mwenye faida kwake binafsi kwa taifa lake na kwa familia yake.
Yote haya ni majibu yaliyo sahihi lakini jibu sahihi zaidi kuhusu dhana hii ya Elimu ni jumla ya maarifa,stadi na mielekeo inayotawaliwa na mila na desturi za jamii ambapo binadamu huweza kupata kwa kujifunza mwenyewe, kufundishwa na kwa njia nyingine.
Mtu mwenye Elimu huwa na taaluma au mbinu ambazo mtu huyo hufuata na kutumia katika kutatua matatizo yanayomzunguka.
Mfumo wetu wa kielimu wengi unatutengeneza kufikiri elimu ni maarifa ya kazi peke yake ambayo yatatupatia kipato. Huku tukisahau kabisa kwamba elimu ni zaidi ya hapo tunapodhania. Tukiishia katika fikra za kwenda shule kusudi tupate kazi na kupata pesa kwa ajili ya matumizi yetu ya kila siku tu, ndipo linapokuja suala la bora Elimu na si Elimu bora.
Elimu bora hukuza ufahamu wa mwanadamu.Ukuaji huu wa ufahamu hupelekea mabadiliko chanya ya mwanadamu huyu kifikra,maono na mitazamo katika jamii inayomzunguka hivyo kumfanya binadamu huyu kutenda katika usahihi kulingana na maadili ya jamii hiyo, na kumfanya mwanadamu huyu kuwa bora zaidi na mwenye kuzalisha kwa faida ya kwake binafsi kwa familia,jamii yake na taifa kwa ujumla.
Elimu bora atakayopata mwanadamu huyu kwanza itamwezesha kuitazama na kuiongoza familia yake vizuri. itamwezesha kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayomzunguka pia na taifa kwa ujumla hivyo kumwezesha kuwa mtu bora na mzalishaji kwa taifa. Ndio msingi wa elimu.
Mwanadamu huyu mwenye Elimu bora tunamtegemea,awe na uwezo wa kuchanganua kati ya mambo yaliyo sahihi na yale yaliyo mapotofu, na ataamua bila kusita kufuata mambo ambayo ni sahihi na kuacha kabisa mambo yaliyo potofu.
Mwanadamu huyu tunategemea atakuwa na uwezo pia wa kutatua matatizo yake yeye mwenyewe,matatizo yanayoikumba familia yake na jamii yake kwa ujumla, mwanadamu huyu ni mtu ambaye mwenye elimu bora.Mwenye uwezo wa kufahamu na kuchanganua mambo na kutenda katika usahihi.
Mwenye uwezo wa kuitazama familia yake vizuri, mwenye uwezo wa kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayomzunguka, mwenye uwezo wa kuwa raia bora na mtu bora ambaye anazalisha katika taifa lake.
Tunapowapa watu elimu yatupasa kuangalia tabia za watu wetu na kuzijenga katika usahihi. ni muhimu elimu yetu pamoja na kuangalia stadi za ufanyaji wa kazi kwao lakini zijenge tabia zao. Hii italeta manufaa kwa taifa na sio hasara. Kama tunawapa stadi za ufanyaji kazi tu watu wetu lakini wanakuwa hawana manufaa kwa taifa letu bali ubinafsi na hasara basi hiyo elimu ina kasoro tuitazame upya.
Elimu bora itamfanya mtu kutenda katika usahihi.Elimu ambayo sisi kama taifa tunapaswa kuijenga. Na watoto wetu watakuwa wenye akili kama wakipata elimu kama hiyo. Ni elimu ambayo itawalinda dhidi ya maangamizi, itawalinda dhidi ya uovu.Lakini pia itawapa ujuzi wa kufanya kazi.
Kwahiyo tukizalisha watu wenye Elimu bora,tutegemee viongozi wazuri, watu wenye ujuzi wa hali ya juu kazini waaminifu na wenye maadili na nidhamu ya kutosha.
Vinginevyo elimu ambayo itampa tu mtu ujuzi wa kazi pasipo mambo mengine ni sawasawa na kutwanga maji kwenye kinu.Elimu bila maadili ni sawasawa na mtu bila kiungo.Haitokuwa na faida. Itapotea tu.
Kuelimika ni kuondokana na matendo ya kijinga yasiyo na faida. Dhana ya elimu ni kuondokana na ujinga. Na tunapima faida ya kitu kutokana na matokeo ya kila matendo tunayofanya. Ili twende mbele kama taifa lazima tuelimike. Tuachane na ujinga na tutende katika usahihi.
Hivyo ni Muhimu sana tunapotoa elimu, kuangalia tabia na dihamu za watu wetu ili kuzijenga katika kutenda kiusahihi. Nidhamu,maadili na uzalendo huleta mwelekeo iwe kwa taifa au kwa mtu binafsi.